GAZUKO KUACHIA KAZI YA PAMOJA NA EDSON MWASABWITE.
Gazuko na Mwasabwite
Ni ujio mpya wa Gazuko Junior au Preacher Gazuko ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake unaoitwa Acha kulia ambao umeingia katika tuzo za Nyimbo za Injili Africa akishindanishwa na waimbaji kutoka nchi mbalimbali za Afrika.
Sasa Preacher Gazuko anakuja na wimbo mpya uitwao Ombi Langu ambao amemshirikisha mwimbaji mahiri wa nyimbo za injili aitwae Edson Mwasabwite ambae anatamba na wimbo uitwao Ni kwa Neema na Rehema.
Wimbo huu (Ombi Langu) umerekodiwa ndani ya studio bora za Tuners Production na siku ya Jumamosi tarehe 16/08/2014 wimbo huu utaanza kusikika rasmi ndani ya vituo mbalimbali vya redio hapa nchini Tanzania pamoja na nje ya nchi..
Edson Mwasabwite na Producer Edwin Mrope
Endelea kumpigia kura Gazuko kupitia http://www.africagospelawards.com/ ili Tanzania iibuke na tuzo kupitia Gazuko...
Gazuko
0 comments:
Post a Comment