Advertisements

Sunday, April 20, 2014

MWIMBAJI MPYA ATANGAZA KUVUNJA CD



                 EZEKIEL YOHANA AKIWA AMESHIKILIA GITA


Mwimbaji anayekuja juu katika tasnia ya muziki wa injili hapa Tanzania anayefahamika kwa jina la Ezekiel Yohana mwenye maskani yake jijini Arusha, Amezungumzia huduma yake ya uimbaji Ezekiel Yohana ambaye pia ni mtunzi na mpigaji wa vyombo kama keybord amesema kuwa ndoto yake pia ni ombi lake kwa Mungu kuwa ifike kipindi aache kuimba muziki kwa kutumia cd na badala yake aanze kuimba laivu kwa kutumia keybord,drums n.k

SABABU ZA EZEKIEL YOHANA KUWAZIA KUIMBA LIVE
hapa Ezekiel akielezea maono yake "unajua kaka mimi ni mwimbaji binafsi lakini pia ni kiongozi wa sifa na kuabudukwahiyo huwa ninaona jinsi Mungu anavyotembea kupitia muziki wa laivu hata ninapopata ujumbekutoka kwa Munguhuwa ni rahisi saana kuunena kwan muziki unaweza ukawa unapigwa kwa chini wakati mimi ninapounena ujumbe husika na baada ya hapo nikaendeleana muziki kama kawaida lakini unapotumia cd au wengi wamezoea kusema kutumia cd inakufunga kwa sababu inakuwa recorded hivyo mwimbaji ukiongezea maneno yanakuwa makelele tu

                                       EZEKIEL AKIPIGA GITAA

                                   HARAKATI ZA KUANZA KUIMBA LIVE
kwakweli muziki wa laivu pamoja na uzuri wake lakini unahitaji gharama saana hivyo nipo katika hizo harakati.......HAYO NDIO ALIYOYASEMA EZEKIEL YOHANA KUPITIA NAMBA ZAKE ZA SIMU AMBAZO NI 0768234141

0 comments:

Post a Comment

Copyright © KANISA MUZIKI All Right Reserved
Designed by Harman Singh Hira @ Open w3.