MAAJABU YA MWIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI NEEMA KAYOMBO
COVER LA ALBUM YA MAAJABU YA YESU (mbele)
Mwimbaji wa muziki wa injili hapa nchini Tanzania mwenye asili ya mkoani Iringa ambaye anafanya vizuri katika radio mbali mbali anayejulikana kwa jina la Neema Sabas Kayombo, leo amefunguka kwa kuelezea wimbo wake wa maajabu ya Yesu ambao ndio umebeba album yake inayoitwa Maajabu ya Yesu yenye nyimbo nane miongoni mwa nyimbo hizo ni jihadharini,mimi ni nani,Mungu ni Roho na nyingine.
COVER LA CD LA ALBUM YA MAAJABU YA YESU
Neema amesema kuwa kitu kilichompelekea kuandika na kurecord wimbo huo wa Maajabu ya Yesu ni kutokana na mambo mengi ambaye Mungu amemtendea kupitia mwanae Yesu kristo pia amesema kuwa album yake ipo tayari hivyo unaweza kumsapoti mwimbaji huyu kwa kujipatia nakala yako wasiliana naye kwa namba hizi 0658173640
Pia mwimbaji huyu yupo tayari kwa mialiko ya kihuduma katika mikutano,semina,matamasha n.k
0 comments:
Post a Comment