Advertisements

Wednesday, June 18, 2014

GAZUKO KUFANYA TAMASHA LA ACHA KULIA.



                                            


Mwana harakati anayekuja juu zaidi hapa nchini Tz katika anga la Gospel hip hop anayekwenda kwa Gazuko amesema kuwa baada ya kuachia video ya wimbo wake wa ACHA KULIA sasa ni muda muafaka wa kukutana na mashabiki wake kwa kuwaandalia tamasha alilolipa jina la ACHA KULIA DAY.

                                                   GAZUKO AKIWA JUKWANI
Tamasha hilo litafanyika siku ya tarehe 29/6/2014 katika ukumbi wa Heros Hotel uliopo buguruni rozana jijini Dar es salaam ambapo umepakana na shule ya Mopac kuanzia mida ya saa nane mchana mpaka kumi mbili jioni hakutakuwa na kiingilio siku hiyo.
Gazuko amesema waimbaji mbali mbali watakuwa mahali pale wakimsapoti kama vile:-
Apostle Bashando,Sir Mbezi,Rungu La Yesu,Leah Amos,Huru kweli,Hugo Mlula,Sammy Kapela,Mophaty Mwanjala,Janeth Ngende,Neema Ng'asha na wengine kibaooooo
Gazuko amewaomba mashabiki wake wafike kwa wingi siku hiyo kwani itakuwa si yakawaida na ni tofauti sana na matamasha mengine ambao yamezoeleka.
kwa mawasiliano na Gazuko piga simu namba 0657985598.
ACHA KULIA DAY MTAZAME YESU.

0 comments:

Post a Comment

Copyright © KANISA MUZIKI All Right Reserved
Designed by Harman Singh Hira @ Open w3.