WARAKA KWA WAIMBAJI WOTE WA MUZIKI WA INJILI
Msanii wa muziki na CEO wa kampuni ya Showbiz Defined Media Company, Make Tee.
Msanii wa muziki na CEO wa kampuni ya Showbiz Defined Media Company,
Make Tee ameandika barua ya wazi kwa Watanzania wanaofanya muziki wa
injili nchini.Barua hiyo inasomeka kama ifuatavyo:
Ninavyojua muziki wa kwaya unauza sana kuliko muziki wowote Tanzania , Matamasha yao yanajaza watu wengi sana kwasababu moja , hayachagui umri na pale watu wengi wanafuata neno la Mungu.
Wajanja wachache walishtukia muda mrefu na kuingia huko wakijidai wanasaidia muziki huo ufike mbali, lakini machache yameanza kuonekana na baadhi ya wanakwaya nilikutana nao na kuongea nao nikagundua propaganda imeanza nako kuwa ya khali ya juu kuliko kwenye muziki huu wa bongo flava
1. Wasambazaji wa Cd/ Tape and DVD
Imetokea kasumba kuwa watu hawanunui tena CD za audio so waimbaji wametakiwa punde wanaporekodi audio lazima wafanye na album ya VIDEO kwa gharama zao ndipo album inunuliwe.
Punde wanapofanya hivyo hao hao wasambazaji wanawaambia waanze na copy chache za majaribio, wengi wamepewa copy zisizozidi 500 na wakiishagonga copy hizo akirudi tena kuulizia anaambiwa mzigo hauendi kabisa na haambiwi kuwa ameuza kopi ngapi, wengine ndio huwa mwisho wa kugonga copy nyingine
Niliuliza swali kwa baadhi ya wanakwaya kuwa “gharama za kuitangaza album kama ipo sokoni ni ya msambazaji au mwanakwaya?” nilijibiwa hata wenyewe hawaelewi, hapa palileta utata kidogo kama biashara ni yenu wote kwanini uhangaike peke yako muimbaji?
2. Utengenezaji wa audio au video
Ukiangalia Kenya na Uganda wanafanya muziki huu wa Gospel very serious na wengi mnaofuatilia mmeona , standard ya video na audio iko juu ingawa pia wapo wanaochemka lakini kwa kiasi kidogo
Wasambazaji wengine hapahapa Tanzania wameanzisha makampuni ya kutengeneza audio na video, muimbaji akitengenezea ambako yeye hataki na ameitengeneza kwa kiwango kinachostahili huwa hawakubali kuingia mkataba wa kusambaza kazi hizi na kutoa kasoro kibao mpaka kupelekea waimbaji kukata tamaa kabisa ya kusambaza neno la Mungu kwa njia ya uimbaji,
3. Mabadiliko
Wengi wanakwaya hamtaki mabadiliko na kuangalia ulimwengu umekuwa watu wanaangalia sana standard ya vitu imefika sehemu tunafanya vitu kwa mazoea, nnachojua Mungu kama amekupa pumzi bure tu kwanini usiitende kazi yake kwa kiwango cha juu?ili neno lake lisambae kote?
4.Muonekano
Kuna Baadhi ya wanakwaya muonekano wao huwezi kutofautisha na wasanii wa muziki wa kidunia, maisha wanayoishi huwezi ukasema huyu ni muimbaji wa Gospel kabisa, kwa hili wapendwa badilikeni
5. Chuki na Dharau
Baadhi ya wasanii waliotoka au wenye majina hawa huwadharau waimbaji wadogo na kutowapa ushirikiano wa kutosha
NINI KIFANYIKE
Nimeeleza mengi hapo juu ila kwa utafiti niliufanya na baadhi ya waimbaji ni kuwa mkiuza kazi zenu kama wasanii wengine wakubwa ambao tunaona wanafanya kwenye matamasha au kwenye makanisa yenu possibility ya kuuza zaidi ya msambazaji ni kubwa zaidi, mfano hai ninao kwa waimbaji wawili ambao mpaka sasa wameuza zaidi ya nakala 2500 za vcd kwenye matamasha wanayokwenda na makanisani baada ya ibada
Washarika ni wengi ambao wapo kwenye madhehebu yenu ambao mkiwaonyesha nia kifasaha nini mnaweza kukifanya wapo tayari kuwasaidia mkafanikiwa hata siku moja msitegemee kuna mtu mwingine zaidi ya unaesali nae au kushinda nae anakujua zaidi akakusaidia.
Kwasababu nimeyaona haya matatizo nimekumbana nayo msisite kuuliza kwa ushauri zaidi nini cha kufanya ili muweze kufikisha neno la bwana kwa njia ya picha, muziki na video
Waimbaji mshirikiane pendaneni ndivyo neno la Mungu linavyosema Mpende jirani yako kama.
CHANZO: BONGO 5
0 comments:
Post a Comment