Advertisements

Monday, April 14, 2014

HAYA NDIO MAISHA YA EDSON MWASABWITE A.K.A MWASABWITE ASILIMIA MIA



              MWASABWITE ASILIMIA MIA AKIWA KATIKA POZI


ilikuwa ni mateso makubwa kwa mwimbaji wa muziki wa injili aliyeanza kutamba na wimbo wa "ni kwa neema tu" lakini sasa anatamba na wimbo wa "ni Mungu tu" anayefahamika kwa jina la Edson Mwasabwite lakini sasa hivi amepewa jina la Mwasabwite Asilimia mia,
KUTOKA KUSHOTO NI MWIMBAJI CHARLZ THOBIAS AKIFUATIWA NA MWANAGOSPEL HIP HOP GAZUKO ALAFU ANAYEFUATA MWASABWITE MWISHO NI BRIAN PEMBENI NI GARI ANAYEIMILIKI MWASABWITE


Mwasabwite Asilimia mia amesema kuwa katika kipindi cha miaka ya nyuma alikuwa akipata mateso ususani kipindi alichokuwa akisoma shule ya msingi kuaznia darasa la kwanza hadi la saba alikuwa akitembea zaidi ya kilometa 10 kwa mguu kila siku kutoka nyumbani kwao kuelekea shule aliyokuwa akisoma....lakini pia haikuishia hapo mateso hayo yalikuja kuzidi zaidi pale alipoanza huduma rasmi ambapo Mwasabwite Asilimia mia anasema kuwa alikuwa akitembea zaidi ya kilimeta 40 na baiskel kwenda kuomba nafasi za kuimba katika mikutano ya injili na wakati mwingine amekuwa akizikosa nafasi hizo
Hayo yalikuwa maisha ya tabu kwake kwa kipindi hicho lakin sasa hivi anamshukuru sana Mungu kwa kusema ni Mungu amemuhurumia kwani sasa anamiliki gari ikiwa ni kitu hakuwahi kuwazia maishani mwake kama atakuja kumiliki Mwasabwite Asilimia Mia sasa hivi ameingiza album yake mpya sokon ya NI MUNGU TU AMENIHURUMIA ASILIMIA MIA
BONYEZA HAPA KUPATA HABARI ZAIDI

0 comments:

Post a Comment

Copyright © KANISA MUZIKI All Right Reserved
Designed by Harman Singh Hira @ Open w3.