JESCER MICHAEL NI CHIPUKIZI WA NYIMBO ZA INJILI, MWENYE KIPAJI CHA KUTUNGA NA KUIMBA, MALENGO YAKE NI KUUFIKIA ULIMWENGU KWA UIMBAJI.
Mkoa wa Dodoma ni kati ya mikoa ambayo kuna waimbaji maarufu wa injili
hapa Tanzania vile vile iko mikoa kama Mbeya, Kigoma, Arusha, Dar na
kwingineko. ukitaja jina kama Rose Mhando ni jina linalojulikana sana na
ni malkia wa nyimbo za injili hapa Tanzania na hata kuweza kuweka
mkataba na kampuni kubwa la mziki hapa Africa.
lakini katika mkoa huu wa Dodoma kuna waimbaji wengi sana ni under
Ground na wengine ndo wana chipukia. Blog hii ilipata nafasi ya kuonana
na baadhi ya waimbaji hao mjini Dodoma na kufanya nao mahojiano kujua
machache katika huduma zao. kama mnavyojua na ni ukweli usio pingika
kuwa kwa sasa mziki wa injili Tanzania umeshika hatamu kuliko miziki
wowote. na hii ni kutokana na umahili na kazi nzuri zinazofanywa na watu
wote katika muziki huu wa Gospel hii ni pamoja na waimbaji, wapigaji
ala za muziki, maproduza wa audio na Video pamoja na wasambaji wa kazi
hizi wamekuwa na mchango mkubwa, hii imeleta kutokea kwa uamusho na kuwa
na waimbaji wengi wanaochipukia na ambao wana fanya vizuri katika
tasnia hii na kuleta changangamoto kwa waimbaji wakongwe.
Jescer Michael ni mmoja ambaye tuliweza kufanya mahojiano mafupi kujua
kwa ufupi amejipanga vip. ni kati ya waimbaji chipukizi wenye kipawa cha
uimbaji, na sauti yenye mvuto ambayo haichoshi kusikiliza. sikiliza
hahojiano hapo chini
Jescer anahitaji watu watakao msaidia kukamilisha albamu yake ambayo
bado anarekodi amekwama fedha za kumalizia basi kama utaguswa unaweza
kuwasiliana nae kwa simu. 0788009030 na 0716584777
au unaweza kumpata facebook https://www.facebook.com/jescer.michael?fref=ts
au unaweza kumpata facebook https://www.facebook.com/jescer.michael?fref=ts
0 comments:
Post a Comment