Advertisements

Monday, April 14, 2014

MWANAMUZIKI WA NYIMBO ZA INJILI ROSE MUHANDO ADAIWA KUSAKWA..! ROHO KIGANJANI.! SOMA KISA HAPA LAIVU BILA KING'AMUZI

Mwanamuziki wa Injili daraja la kwanza nchini, Rose Muhando.
Stori: Erick Evarist
MY GOD! Mwanamuziki wa Injili daraja la kwanza nchini, Rose Muhando anaishi roho mkononi kufuatia madai kwamba kuna watu wanaomsaka wakisemekana wametumwa kuichukua roho yake, Ijumaa Wikienda lina kisa kizima.


Kwa mujibu wa chanzo makini, Rose anaishi kwa machale jijini Dar akikimbia Dodoma baada ya taarifa kwamba mtu mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Nasani na wenzake wanataka kumdhuru kama si kumtoa roho kabisa.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama aliyepata ajali inayohusishwa na watu wenye nia ya kutaka kumteka Rose Mhando.

“Hao watu si wazuri! Mara kwa mara wamekuwa wakiandaa mikakati ya kumfanyia kitu kibaya Rose.
“Mfano mzuri ni Aprili 3 na 4, mwaka huu, watu hao waliweka mtego wa kumteka Rose kwenye hoteli moja jijini Dar es Salaam, wakashindwa kutokana na mazingira,” kilisema chanzo hicho.

Alex Msama akiwa amelazwa mara baada ya kupata ajali.

TUKIO BICHI
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kuwa baada ya watu hao kushindwa kufanikisha zoezi hilo siku mbili hizo, Aprili 6 (mwaka huu) walijipanga tena kumvamia Rose katika tamasha la Injili alilolifanya kwenye Kanisa la KKT-Usharika wa Magomeni-Mapipa jijini Dar.

“Tulisikia kuwa kuna watu wametumwa, wakafikia katika gesti moja iliyopo Magomeni Mwembechai (jina lipo) lakini walishindwa kutekeleza azma yao hiyo kwani tayari timu ya Rose ilishapewa taarifa hivyo akajiandaa. Pia waliogopa zaidi baada ya kumwona mtu mmoja amekaa meza kuu akiwa amevalia mavazi ya kijeshi, tena mwenye cheo cha juu maana alikuwa na nyota begani,” kilisema chanzo.

Kikaongeza: “Siku hiyo timu ya Rose haikuripoti polisi juu ya tukio hilo kwani tayari walishawahi kutoa taarifa kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu baada ya Rose kutishiwa maisha na huyo Nasani.”

CHAMA CHA WAIMBA INJILI CHAPEWA TAARIFA
Taarifa zaidi zilidai kuwa uwepo wa taarifa za Rose kutaka kutekwa Magomeni zilimfikia Katibu wa Chama cha Waimba Injili Tanzania, Stella Joel ambaye naye alipoongea na gazeti hili alikiri kuzipata hizo.

Stella: “Tulisikia mapema kwamba kuna watu wametumwa kuja kumteka Rose. Tamasha siku hiyo lilianza saa nane mchana lakini sisi tulituma ‘mashushushu’ wetu saa tatu asubuhi kukagua mazingira. Kweli, wakati tamasha limeanza kuna muda waliingia watu watatu, wakaangazaangaza huku na kule kisha wakatoka.

“Tunamshukuru Mungu hakuna jambo baya lililotokea ingawa tulikaa kwa tahadhari kubwa,” alisema Stella.
Paparazi: Tunasikia walikuta mwanajeshi wa cheo cha juu amekaa meza kuu wakaogopa, ni kweli?
Stella: Hapana, yule si mwanajeshi. Ni muimba Injili anaitwa Mwanamapinduzi. Huwa anapenda kuvaa kama mwanajeshi.

AJALI YA MSAMA YAHUSISWA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga madai zaidi kwamba hata ajali aliyoipata Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama mkoani Dodoma, Ijumaa iliyopita, ilipangwa na huyo Nasani. Habari zinadai kwamba Nasani hakupenda Rose ashiriki katika Tamasha la Pasaka linaloandaliwa na Kampuni ya Msama kwa sababu yeye ana bifu naye.

Ilidaiwa kuwa, Machi 8, mwaka huu Nasani na Msama walifanya kikao cha kujadili Rose atoke kwenye Tamasha la Pasaka, lakini muandaaji huyo alikataa.

ROSE NA NASANI KUNA NINI?

Ikaendelea kudaiwa kuwa miaka kadhaa iliyopita, Rose na Nasani waliwahi kufanya biashara ya pamoja (haikutajwa) lakini waliposhindwana hawakuachana vizuri na ndiyo maana jamaa huyo amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha anamdidimiza mwimbaji huyo mahiri Bongo.

NASANI ANASEMAJE?
Juzi paparazi wetu alimtafuta Nasani kwa njia ya simu, alipopatikana alisema:
“Hilo tukio la Rose kutaka kutekwa ndiyo nalisikia leo. Sasa mimi nimteke Rose ili iweje? Siwezi kufanya hivyo na wala sihusiki kabisaaa.

“Kuhusu ajali, siku moja kabla ya tukio mimi nilikuwa na Msama, akaniambia anakwenda Dodoma, mimi nikamwambia nitaondoka saa 5:20 na basi asubuhi yake, yeye alitangulia kwa gari binafsi. Nilipofika Chalinze, mke wake akanipigia simu na kuniambia mumewe amepata ajali, sasa hapo mimi nahusikaje?
“Nahisi kuna watu wananizushia mambo ili kunichafulia jina langu maana kuna meseji za vitisho nimetumiwa.

KUHUSU ROSE
Kwa mujibu wa Stella, Rose alisema yeye anamuamini Mungu kuwa hakuna atakayeweza kumuangusha lakini pia anajivunia uwepo wa taarifa zake kwa IGP.

Kuhusu tukio la Magomeni, Rose alisema hajui chochote labda kwa vile alikuwa akipafomu jukwaani.
Hata hivyo, juzi paparazi wetu alimpigia simu Rose mara tatu bila kupokelewa. Mara ya nne ilipokelewa, lakini mawasiliano yakawa mabovu.

SOURCE ; MASAI NYOTAMBOFU.
BONYEZA HAPA CHINI KWA HABARI ZAIDI
https://www.facebook.com/profile.php?id=100008158600958 

0 comments:

Post a Comment

Copyright © KANISA MUZIKI All Right Reserved
Designed by Harman Singh Hira @ Open w3.